Msanii wa muziki Madee leo anaungana na mama yake kwenda
kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na watoto yatima wa kituo cha Hope
kilichopo Kibaha Maili Moja, Mkoa wa Pwani.
Madee amesema kuwa ameamua kufanya hivyo kama sehemu ya kuirudishia jamii na kumshukuru Mungu.
“Naelekea Kibaha kwenda kukaa na mama yangu na familia yangu pia. Kwa
ujumla kuna kituo pale kinaitwa Hope cha watoto yatima,nitatoa kile
ambacho nimekipata mwaka mzima. Kwahiyo naona ni muhimu kushukuru
kwasababu ninaweza nisifike mwakani. Lazima kushare na watu wengi furaha
yako.Baadaye baadae tutatoa taarifa tunakutana wapi. Lakini najaribu
kuongea na Marco Chali ambaye ni rais wa Mbudya, aniunganishe kule.
Namshukuru Mungu, wadau wote wa muziki pamoja na mashabiki wangu kwa
kunifikisha hapa.”

Post a Comment