
WALIMU WA AJIRA MPYA 2014 WALIOKUBALIWA KUBADILISHIWA VITUO
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imefanya
mabadiliko ya vituo vya kazi kwa walimu Ajira mpya mwaka 2014 baada ya
kupokea na kuchambua maombi mbalimbali kutoka kwa walimu walioomba
kubadilishiwa vituo.
Hivyo
walimu wote walioomba kubadilishiwa vituo lakini majina yao hayapo
katika orodha hii kwa ngazi zote watambue kuwa maombi yao
hayakukubaliwa na hivyo wanatakiwa kwenda kuripoti katika vituo
walivyopangiwa kwa mujibu wa tangazo la tarehe 15/03/2014.
Inasisitizwa kuwa tarehe ya mwisho ya kuripoti ni 10/04/2014 na
ambaye hataripoti mpaka tarehe hiyo atakuwa amepoteza nafasi ya ajira.
Hakutakuwa na mabadiliko mengine tena.
Tunawatakia kila la kheri.
- Walimu wa Cheti (Daraja IIIA) Kwa Ajili Ya Shule Za Msingi (Bofya hapa)
- Walimu wa Stashahada Kwa Ajili Ya Shule za Sekondari (Bofya hapa)
- Walimu wa Shahada Kwa Ajili Ya Shule Za Sekondari (Bofya hapa)
Chanzo cha taarifa hii: pmoralg.go.tz
Post a Comment