Makalio madogo kikwazo Venezuela

Wanawake nchini Venezuela wanatumia kemikali haramu kuongeza ukubwa wa makalioyao na kujiletea madhara makubwa ya kiafya
Hii ni kutokana na mtindo ambao unaonekana na wengi nchini humo kwamba mwanamke mwenye makalio makubwa ndiye anayependeza zaidi
Wanawake wengi sasa wanahatarisha afya zao kwa kutaka kuwa 'warembo'
Akiwa anabubujikwa na machozi , mwanamke kwa jina Denny anakumbuka vyema alivyoamuka siku moja na kujipata na uvimbe sawa na ukubwa wa mpira katika sehemu ya chini ya mgongo wake.
Hangeweza kutembea wala kuinama na uchungu ukawa mwingi kupita kiasi.
Hata kabla ya kumwona daktari, Denny, mwenye umri wa miaka 35 ambaye pia ni wakili, alijua kuwa hiyo ilikuwa athari ya kudungwa kemikali ijulikanayo kama 'silicon' , ili kuongeza ukubwa wa makalio yake.
Uvimbe huo ulisonga hadi katika sehemu ya chini ya mgongo wake na kuanza kuumiza uti wake wa mgongo. Yote kwa sababu ya kutafuta urembo.
"nilishtuka sana . Singeweza kutembea na hivyo ndivyo masaibu yangu yalivyoanza, ''alisema Denny.
Sindano ambazo wanawake hujidunga ili kuongeza ukubwa wa makalio , ni moja ya mbinu ya kujiongeza urembo ambayo wanawake wengi wamebugia nchini Venezuela.
Daktari anaonyesha picha ya moja ya athari za sindano za Silicon kwa makalio
Sababu? Kupata kile ambacho jamii inaona kama urembo.
Sindano hizo zilipigwa marufuku na serikali mwaka 2012, miaka sita baada ya Denny kudungwa.
Denny alidungwa sindano ya kemikali hiyo ya Silicon mwaka 2006 na leo ndio ameanza kuhisi athari zake.

Miaka 18-50

Hata hivyo wanawake wengi wanaendelea kujiongezea makalio. Takriban asilimia 30 ya wanawake walio kati ya umri wa miaka18 na 50 wanatumia Silicon kuongeza ukubwa wa makalio yao.
Wanawake wanavutiwa na mbinu hii ya kuongeza ukubwa wa makalio kwa sababu bei yake ni nafuu. Lakini madhara yake ni amkubwa mno.
Madaktari wanasema kuwa kemikali hii husambaa mwilini na pia inaweza kuathiri kinga ya mwili.
Madaktari wanamfanyia upasuaji mwanamke aliyepatwa na madhara ya sindano za Silicon
Utafiti unaonyesha kuwa wanawake zaidi ya kumi hufariki kila mwaka kutokana na kudungwa sindano hizo.
Kuna madaktari wawili pekee wanaoweza kumfanyia upasuaji mtu kama Danny aliyeathrika kutokana na kemikali hiyo lakini kwa Danny anahitaji kusubiri kwa mwaka mmoja kabla ya kufanyiwa upasuaji huo maana kuna wanawake wengi kwenye orodha ya wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.
Wanawake wengine wanasema kuwa wanalazimika kuongeza ukubwa wa makalio kutokana na shinikizo za wapenzi wao. Lakini madhara yanapowakuta , ni wao wanaoteseka zaidi.
Astrid de la Rosa ambaye sasa ni mwanaharakati anayepinga sindano hizo,anasema yeye hakujua kama mwanamume angeweza kumfanya akaoengeze ukubwa makalio yake.Nusura amuache
Lakini madhara yalimpmata walati kinga yake ya mwili ilianza kuathirika baada ya kudungwa sindano hiyo na kuwa na makali makubwa..
Wanaharakati nchini Venezuela wanataka serikali ichukue hatua kali zaidi dhidi ya wanaowadunga wanawake sindano hizo za 'Biopolymer.'
Waigizaji , wanaume kwa wanawake, wanamitindo , wote hawa wanataka kupendeza na hivyo hudungwa sindano hizo nchini Venezule, lakini madaktari wanaonya kuhusu madhara yake ambayo ni makubwa mno
- Bbc

Post a Comment

أحدث أقدم