Mama
anayetuhumiwa kwa mauaji ya watoto wake watatu nchini Uingereza amewekwa
rumande kwa ukaguzi wa kiakili kubaini ikiwa alikuwa timamu wakati wa
mauaji hayo.
Tania
Clarence, mwenye umri wa miaka 42, alihudhuria kikao cha mahakama kwa
njia ya video akiwa gerezani akituhumiwa kwa mauaji mapacha wake wawili
wenye umri wa miaka mitatu na mwanawe msichana mwenye mwiri wa miaka
minne.
Mahakama
pia ilisikia kuwa watoto hao walikuwa na ulemavu uliosababishwa na
ugonjwa wa uti wa mgongo.Watoto hao walemavu, walipatikana nyumbani kwao
katika mtaa wa New Malden wakiwa wamefariki Aprili 22.
Mahakama iliambiwa kuwa watoto hao walifariki katika hali ya kuzuiwa kupumua.
Jaji
Judge Brian Barker, alisema Bi Clarence anaweza kuondolewa jela na
kuwekwa rumande kufanyiwa uchunguzi na kupokea matibabu ya kiakili kwa
sababu tukio hilo sio la kawaida
''Hio sio
dhamana , lakini ninachoamrisha ni aweze kufanyiwa ukaguzi wa kiakili
kuambatana na kifungu cha 35 cha sheria. Baada ya hapo anaweza kuwekwa
rumande ili achunguzwe zaidi hali yake, '' alisema jaji.
Wendesha
mashitaka waliambia mahakama kuwa polisi walikuwa wanasubiri matokeo ya
uchunguzi wa maiti za watoto kabla ya kubaini chanzo cha vifo vyao.
Mahakama iliambiwa kuwa babake watoto hao alikuwa nchini Afrika Kusini na mwanao mkubwa wakati wa mauaji hayo.
Mahakama itasikia baadaye utetezi wa Bi clarrence ikiwa anakiri au kukana mauaji tarehe 15 mwezi ujao.
إرسال تعليق