Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi,
Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea Aprili 22, mwaka huu ,
saa 12 jioni kijijini Mnyagala.

Walikuwa
ni wakazi wa kijiji hicho kilichopo katika Tarafa ya Kabungu wilayani
Mpanda katika Mkoa wa Katavi na walipigwa na radi wakati wakirejea
nyumbani kutoka kwa jirani yao.
Alisema walikwenda kwa jirani yao
kumsalimia na ghafla wingu dogo la mvua lilitanda na kulazimu
kuondoka kuwahi kurudi nyumbani wasinyeshewe mvua.
"Wakati wakiwa
njiani wakielekea nyumbani kwao walipofika jirani na nyumba yao
umbali wa meta 15 ndipo walipopigwa na radi na kufa papo hapo. Mama
alijeruhiwa vibaya na radi hiyo kifuani na bintie alijeruhiwa
vibaya kichwani," alisema Kamanda Kidavashari.
إرسال تعليق