Maonyesho ya Vyuo Vikuu Zanzibar Kuadhimisha Miako 50 ya Muunganowa Tanganyika na Zanzibar.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Elimu Chukwani akitowa maelezo kwa wananchi wanaotelea banda lao na kutowa maelezo ya elimu ya Sayansi viumbe vya baharini na nchi kavu. 

Mwanafunzi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Zanzibar akitowa maelezi jinsi ya kuandaa seti ya vyombo katika meza kwa ajili yawageni katika kupata Chakula mahotelini. 
Mwanafunzi wa Chuo cha Afya Mbweni, kitengo cha Meno, akitowa maelezo jinsi ya kutunza meno na sababu za kusababisha meno kuoza,wakati wa maonesho ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Zanzibar katika viwanja vya Wizara ya Habari Kikwajuni Zanzibar.
Mwanafunzi wa Chuocha Afya Mbweni kitivyo cha Utabibu, akitowa ushauri juu ya Afya ya Wananchi waliofika kutembelea banda lao katika maonesho ya Vyuo Vikuu vya Zanzibar, ikiwa ni kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. yalioandaliwa na Umoja wa Vyuo Vikuu Zanzibar.
Wanafunzi waliofika katika banda la Chuo cha Afya Mbweni, walipata fursa ya kupima afya zao kucheki malaria, katika maonesho hayo. 
Mwanafunzi wa Chuocha Zanzibar School for Health, akimpima Presha Mwananchi aliyefika kutembelea banda la Chuo hicho katika maonesho ya Vyuo Vikuu vya Zanzibar,maonesho hayoyanafanyika katika viwanja vya Wizara ya Habari Kikwajuni Zanzibar.
Mwanafunzi wa Chuo cha Kilimo Kizimbani akitowa maelezo kwa wananchi waliotembelea maonesho hayo katika banda lao jinsi ya Unga wa Muhogo unavyotumika kwa kufanyia Keki na vitu vyengine kwa kutumia unga huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post