Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Elimu Chukwani akitowa maelezo kwa wananchi
wanaotelea banda lao na kutowa maelezo ya elimu ya Sayansi viumbe vya
baharini na nchi kavu.
Mwanafunzi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Zanzibar akitowa maelezi jinsi ya
kuandaa seti ya vyombo katika meza kwa ajili yawageni katika kupata
Chakula mahotelini.
Mwanafunzi wa Chuo cha Afya Mbweni, kitengo cha Meno, akitowa maelezo
jinsi ya kutunza meno na sababu za kusababisha meno kuoza,wakati wa
maonesho ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Zanzibar katika viwanja vya
Wizara ya Habari Kikwajuni Zanzibar.
Mwanafunzi wa Chuocha Afya Mbweni kitivyo cha Utabibu, akitowa ushauri
juu ya Afya ya Wananchi waliofika kutembelea banda lao katika maonesho
ya Vyuo Vikuu vya Zanzibar, ikiwa ni kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar. yalioandaliwa na Umoja wa Vyuo Vikuu Zanzibar.
Wanafunzi waliofika katika banda la Chuo cha Afya Mbweni, walipata fursa
ya kupima afya zao kucheki malaria, katika maonesho hayo.
Mwanafunzi wa Chuocha Zanzibar School for Health, akimpima Presha
Mwananchi aliyefika kutembelea banda la Chuo hicho katika maonesho ya
Vyuo Vikuu vya Zanzibar,maonesho hayoyanafanyika katika viwanja vya
Wizara ya Habari Kikwajuni Zanzibar.
Mwanafunzi wa Chuo cha Kilimo Kizimbani akitowa maelezo kwa wananchi
waliotembelea maonesho hayo katika banda lao jinsi ya Unga wa Muhogo
unavyotumika kwa kufanyia Keki na vitu vyengine kwa kutumia unga huo.
إرسال تعليق