Mchezaji namba sita kwa ubora duniani katika tennis upande wa
wanawake, Maria Sharapova amemshinda Ana Ivanovic na kunyakua taji la
Porsche Tennis Grand Prix kwa mara ya tatu huko Stuttgart.
Mrusi huyo, 27, alishinda kwa 3-6 6-4 6-1 na kushinda taji lake la 30.
Katika hatua nyingine mchezaji namba mbili wa tennis duniani kwa
wanaume, Novak Djokovic ametangaza kuwa yeye na mchumba wake Jelena
Ristic wanatarajia kupata mtoto. ‘Jelena is pregnant!!! We will be
parents soon! #blessed’

Wawili hao wamekuwa pamoja kwa takriban miaka tisa.
إرسال تعليق