Kwenye kipindi cha Nipashe cha Radio One Stereo (audio ake imepachikwa
hapo chini), Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni mmoja wa
wanaounda kundi la UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) Mhe. James Mbatia
(NCCR-Mageuzi) anazungumzia sababu ya baadhi ya Wajumbe kutoka nje ya kikao cha Bunge hilo hapo jana jioni na kususia vikao vinavyoendelea.
Pia amezungumzia kuhusu mipango ya kuwaendea wananchi ili kuwafahamisha sababu ya hatua hiyo.
Leo hii, baadhi ya Wajumbe hao watazungumza na wanahabari mjini Dodoma ili kutoa taarifa yao.
Bofya hapa kusikiliza
إرسال تعليق