Maandamano yakiwa yameanza kuelekea ukumbi wa Mlimani City
Mmoja
ya Waandamaji wa siku ya kumbukumbu ya mauaji ya Rwanda ikiwa imetimia
Miaka 20 akiwa amebeba Mwenge Maalum kwa ajili ya Maadhimisho.
Maandamano
ya Kumbukumbu ya miaka 20 ya Mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994
yakiendelea kuelekea Ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya Maadhimisho
hayo.
Baadhi
ya Wanafunzi pamoja na watu wengine mbalimbali wakiwa wameshika mabango
mbalimbali yanayo elezea siku ya kumbukumbu ya Mauaji ya Rwanda
yaliyotokea Mwaka 1994
Maandamano
yakiwa yamewasili nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City kwa ajili
ya kukabidhi Mwenge huo kwa Mgeni rasmi Mh. Profesa Mark J. Mwandosya
Waziri Ofisi ya Rais.
Mgeni Rasmi Mh. Profesa Mark
J. Mwandosya Waziri Ofisi ya Rais akipokea Mwenge Maalum wa Kumbukumbu
ya Miaka 20 ya Mauaji ya Rwanda kutoka kwa Mustapha Issa wa kwanza
kutoka upande wa kushoto pamoja na Amina Mtegeti.
Mshehereshaji
wa maadhimisho ya kumbukumbu za Miaka 20 ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda
Usia Nkhoma Ledama kutoka UNIC Dar es Salaam, akizungumza jambo kwenye
sherehe hizo.
Baadhi ya wageni waliofika katika kumbukumbu hizo wakiwa wanaimba nyimbo mbili za Taifa kutoka Rwanda na Tanzania.
Mchungaji
Safari Paul akiendesha Maombi Maalum kwa ajili ya Kumbukumbu ya Miaka
20 ya Mauaji ya Rwanda ambapo zaidi ya watu Milioni Moja waliuawa.
Sheigh Othman akiomba dua Maalum kwa ajili ya Miaka 20 ya kumbukumbu ya Mauaji ya Rwanda.
Mgeni
Rasmi Mh. Profesa Mark J. Mwandosya Waziri Ofisi ya Rais akipokea
Mwenge Maalum wa Kumbukumbu za Miaka 20 ya Mauaji ya Rwanda kwa ajili
ya kuwasha Mishumaa ili kuwakumbuka wale wote waliopoteza Maisha.
Akiwasha Mshumaa kwa ajili ya kumbukumbu ya Miaka 20 ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda.
Aliyekuwa
katibu Mkuu wa Saba wa Umoja wa Afrika Dk. Salim Ahmed Salim akiwasha
Mshumaa kwa ajili ya Kumbukumbu ya Miaka 20 ya mauaji Kimbari ya Rwanda.
Mmoja
wa wahimizaji wa Amani na Upendo Amina Mtengeti akiwa anazungumza Jambo
wakati wa Maadhimisho ya Miaka 20 ya kumbukumbu ya Mauaji ya Rwanda.
International
Criminal Tribunal for Rwanda (ICTR) Registrar, Ndugu Bongani Majola
akizungumzia kwa kifupi juu ya Mauaji ya Rwanda ambapo sasa ni Miaka 20
tangu yalipo tokea
Wanafunzi wakiimba wimbo maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya Mauaji ya Rwanda
Mwakilishi
kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon , Mh. Dk
Jamal Gulaid akisoma Ujumbe wa Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.
Mh. Benjamin Rugangazi akitoa Neno kutoka Ubalozi wa Rwanda Nchini Tanzania
Zainab Abdallah kutoka Youth of United Nations akisoma Shairi maalum wakati wa kumbukumbu za Miaka 20 ya mauaji ya Rwanda.
Mgeni
Rasmi Mh. Profesa Mark J. Mwandosya Waziri Ofisi ya Rais akitoa
hotuba yake kwa wananchi waliofika katika Maadhimisho hayo ya Miaka 20
ya Mauaji ya Rwanda.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Swaumu
Vuzzo akitoa neno la Shukurani kwa wageni waalikwa waliohudhuria
maadhimisho hayo.
Baadhi
ya mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, wadau
mbalimbali wa mashirika ya Kimataifa na Sekta binafsi waliohudhuria
maadhimisho hayo.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika Kumbukumbu maalum ya Miaka 20 ya Mauaji ya Rwanda.
إرسال تعليق