Naibu Mkurugenzi wa Habari -CUF Taifa Ndg.Abdul Kambaya akionesha barua
waliopewa na jeshi la Polisi Zanzibar kuahirisha kwa mkutano wao
uliokuwa ufanyike leo jumatano na kuahirisha hadi tarehe 30-4-2014,
mkutano huo na waandishi umefanyika katika Ofisi za CUF Vuga.
Naibu Mkurugenzi wa Habari -CUF Taifa
Ndg.Abdul Kambaya, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo
mbalimbali kuhusiana na kuahirishwa kwa mkutano wao na kufanyika
mwishoni mwa mwezi huo na kufanyika katika viwanja vya kibandamaiti.na
kusema wameridhika na kauli iliotolewa na Jeshi la Polisi Zanzibar
kuhusiana na sherehe za Muungano kutimia miaka 50.
Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Ndg. Hamad Yussuf, akifafanua jambo wakati wa
mkutano na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar,
uliofanyika katika Afisi za CUF Vuga.
Waandishi wa Habari wakiwasikiliza Viongozi wa Vyama vya Upinzani
kuhusiana na mkutano wa Ukawa uliofanyika katika Ofisi za CUF Vuga.
Katibu Mkuu wa BAVICHA Ndg. Deogratias Munishi akizungumza katika
Mkutano huo na waandishi wa habari kuhusiana na Mkutano wa Ukawa katika
viwanja vya Kibandamaiti.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF,akizungumza katika mkutano huo na kutowa
maelezo ya matayarishi ya Mkutano huo wa Ukawa unaotarajiwa kufanyika
katika viwanja vya kibandamaiti wiki ijayo 30-4-2014.
Waandishi wakifuatilia mkutano huo wa Viongozi wa Ukawa wakizungumza na
waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi yaCUF Vuga Zanzibar.
إرسال تعليق