Mushi alitoa kauli hiyo jijini Dar es
Salaam juzi, alipofungua semina ya siku moja ya watendaji na wenyeviti
hao kutoka Tarafa ya Ukonga, iliyokuwa na lengo la kuwapa elimu juu ya
suala zima la ukusanyaji wa mapato hayo.
Alisema ili kufikia malengo
ya ukusanyaji wa mapato kwa asilimia mia moja yaliyowekwa na wilaya
hiyo, kila mtendaji hana budi kujipima kutokana na utendaji wake hatua
aliyosema pia itamsaidia kutoa elimu kwa wananchi wanaomzunguka katika
eneo lake.
“Nyinyi kama viongozi mnapaswa kujituma ili malengo
yaweze kufikiwa na kubwa zaidi itakuwa vizuri kama mtaweka mbele suala
la uaminifu wakati wa ukusanyaji wa mapato hayo vinginevyo hakuna
mafanikio yoyote yanayoweza kufikiwa,” alisema Mushi.
Aidha alisema
malengo ya wilaya hiyo ni kuongoza katika maeneo mbalimbali dhidi ya
wilaya zingine zote na hivyo kuwa mfano jambo alilosema litafanikiwa
kama viongozi hao watajituma na kuzingatia ushauri unaotolewa kwao.
“Tunataka
wilaya yetu iwe ya mfano katika ulinzi na usalama ili watu waweze
kuishi kwa amani, hivyo ili iwe salama ni vizuri kuwandaa watu kuanzia
sasa kwa kuwa thamani ya mtu hupanuka kwa kuongeza upeo wake tuna kila
sababu kutia mkazo katika suala hili la Matokeo Makubwa Sasa kielimu ili
tufike huko,” aliongeza Mushi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya
Fedha kutoka wilaya hiyo, Stellah Mgumia aliwataka watendaji na
wenyeviti hao kusimamia vyema suala zima la ukusanyaji wa mapato ili
kuiwezesha wilaya hiyo kufikia malengo waliyojiwekea.
Alisema lengo
la Serikali kurejesha suala la ukusanyaji kodi za majengo katika
halmashauri, lilitokana na maombi yaliyokuwa yametolewa na halmashauri
hizo, hivyo wanapaswa kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kuonesha kwa
vitendo dhamira yao ya kulitaka hilo.
Alisema ni jambo la fedheha
kuiona baadhi ya mitaa inasuasua katika ukusanyaji wa kodi hizo, jambo
alilosema linatia shaka kufikiwa kwa malengo waliyojiwekea.
إرسال تعليق