Ataweza? Mourinho akiongea na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa leo usiku dhidi ya PSG
Ndani au nje? Eto'o (kulia) akizungumza na Fernando Torres pamoja na Ramires katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea wa Cobham
Jose Mourinho akiwa mazoezini na wachezaji wake jana
MTEGO!. Jose Mourinho amewata wachezaji wake kuwa na imani ya kuitupa nje Paris Saint-Germain katika mchezo wao wa marudiano wa robo fainali usiku wa leo .
Mourinho
amesisitiza kuwa kikosi chake kinaweza kupindua matokeo ya kufungwa
mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza, hivyo mashabiki wawe na imani kwa
wachezaji wao katika kipute hicho kitakachopigwa uwanja wa Stamford Bridge
"Kama Paris watatolewa itawauma sana. Kama tutatolewa ndio kitu ambacho watu wengi wanatarajia"
"Nadhani baada ya mechi
zote mbili tutakuwa na mabao mengi kuliko wao. Kama sina imani hiyo,
sina sababu ya kwenda kwenye mechi na ninafuraha ya kwenda". Alisema
Mourinho.
- Naye Kocha wa PSG, Laurent Blanc amesema hawaogopi kukabiliana na Chelsea Stamford Bridge, hivyo mashabiki wao wajiandae kupokea matokeo mazuri.
Post a Comment