Mr & Mrs Carter, £100K kwa ajili ya Kim na Kanye’s Honeymoon.

beyonce-jay-z-nets-game-11042012-09-435x580
Wiki chache zilizopita Mr & Mrs Carter (Jay Z na Beyonce) walitangaza kuwa hawatahudhuria harusi ya “KimYe” (Kanye West na Kim Kardashian) itayofanyika Siku ya tarehe 24 ya mwezi ujao sababu ya kutokutaka kuonekana katika kipindi cha ‘Keeping up with the Kardishians’ .
Habari mpya kutoka kwa Carters Family ni kwamba amepanga kutumia zaidi ya “£100.000″ kwa kukodi Yatch binafsi ambayo Kanye na Kim watafanyia Honey Moon yao. Yatch hiyo itakodiwa kutoka katika kampuni moja kubwa huko nchini Ufaransa ambako ndipo ndoa ya wawili hao itafanyika. Habari nyingine kutoka kwa watu wa karibu wa Jay Z zinasema kuwa rapper huyo anampango wa kumfanyia party kubwa rafiki yake huyo wa karibu Kanye mara tu atapotoka katika Honey Moon yake na party hiyo itafanyika ndani ya club anayomiliki Jay Z iitwayo club 40/40 mjini Manhattan New York.
Kanye na Jay Z wamekua marafiki kwa mda mrefu sana na hata KIM na Beyonce inadaiwa kuwa sio marafiki sana kihivyo. Tovuti ya Radar Online siku chache zilizopita iliripoti kuwa Kim na Beyonce walikutana katika CLINIC moja ya watoto huko New York lakini Beyonce alionekana kama anampotezea Kim.

Post a Comment

أحدث أقدم