Msanii wa Kenya ‘Fat-S’ anusurika kifo kwenye ajali ya basi iliyokuwa inatoka Dar – Mombasa leo, wawili wamepoteza maisha.

947101_395580443892790_976035035_n Msanii wa Mombasa nchini Kenya, Fat-S aka Mtoto wa Nyanya amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya basi asubuhi ya leo lililokuwa likitoea Dar es Salaam kuelekea mjini Mombasa.


Fat-S

Basi hilo liliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya watu wawili pamoja na kujeruhi abiria 10. Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mkata na Goba, barabara kuu ya Chalinze Segera.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, mtangazaji wa Pwani FM ya Mombasa, Gates Mgenge Grandsona ameandika:
Msanii wa Hapa Mombasa Fat-S mtoto wa nyanya akiwa Bongo(Tz) akirudi Kenya leo hii inasemekana amepata ajali ya gari na walio kuwemo ndani ya gari hilo inaripotiwa wengine wameaga dunia lakini msanii Fat-S amepata majeraha ya vyoo katika mikono yake na miguu kwa sasa inasemekana amepelekwa hospitali.

Post a Comment

Previous Post Next Post