Wakati
wakrito duniani leo kusherekea sikukuu ya kufufuka kwa Yesu
Kristo,Pasaka kwa namna mbalimbali, mtoto wa umri zaidi ya miezi miwili
ametekelezwa na mama yake katika Hopitali ya Rufa Mkoa ya Iringa jana
saa 3 usiku wa kuamkia leo.
Mtoto wa
kike wa zaidi ya miezi miwili mwenye uzito wa kilo tano (5kg)
ametelekezwa katika hospitali ya rufa ya mkoani wa Iringa jana saa 3
usiku wakuamkia leo na mama mmoja na kutokomea kusikojulikana na sasa
mtoto amelazwa katika wodi namba 2 kwa uangalizi zaidi. Mtoto huyo
anahitaji masaida jamii wa hali na mali ili aweze kusherehekea Pasaka
ili afufuke pamoja na Yesu Kristo mkombozi wa ulimwengu. (PICHA: FRIDAY SIMBAYA/MJENGWABLOG.COM/0755528409)
Muuguzi
Msaidizi katika wodi ya watoto namba 6, hospitali ya rufa ya mkoa wa
Iringa, Olipa Gideon Nyagawa akiwa amembeba mtoto huyo kabla ya kupeleka
kwa doktari OPD kwa uchunguzi zaidi baada ya kuona hali ya mtoto
inabadilika kwa kuchemka.
Tabibu
Mkuu wa hospitali ya rufa mkoani Iringa Dkt. M.M. Ndomba akimchunguza
afya mtoto huyo aliyetelekezwa na mama yake hospitalini hapo.
Hawa ni
mmoja ya wasamalia wema waliyojitolea kumpatia baadhi ya nguo alizovaa
mtoto huyo asubuhi leo baada ya kuguswa na tukio hilo la mama
aliyetekekelezwa, walipo kwenda kuwajulia hali wagonjwa mbalimbali
hospitalini leo asubuhi. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
إرسال تعليق