Leo April 17, kifo cha aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa muziki
wa Taarab nchini, Fatuma binti Baraka maarufu kama Bi. Kidude kimetiza
mwaka mmoja.
Bi. Kidude alifariki kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya sukari na uvimbe kwenye kongosho.
“Kwa ufupi alilazwa kipindi kirefu na baadaye akatolewa, lakini
baadaye akaja kuendelea kuumwa tena tukampeleka hospitali tukawa
tunampeleka kwenda na kurudi hapa juzi akaanza kuzidiwa tena tukampeleka
hospitali moja inaitwa Keeni (???) Kwaajili ya matibabu zaidi na drip
na vitu vingine lakini baadaye baada ya siku ya tatu mwenyezi Mungu
akachukua roho yake,” mjukuu wa Bi Kidude aitwae Omar amesema,
siku kama ya leo mwaka jana.
Msiba wa marehemu Bi. Kidude haukuwa wa Tanzania tu bali ni wa dunia
nzima. Mashirika makubwa ya utangazaji duniani yaliwahi kufanya naye
mahojiano kutaka kupata historia yake ya kuvutia. Mwaka jana kituo cha
CNN kilimtembelea Bi. Kidude nyumbani kwake Zanzibar na kumhoji.
Mtangazaji wa CNN aliyefanya naye mahojiano kwenye kipindi cha Inside
Africa, Errol Barnet ni miongoni mwa watu waliosikitishwa na msiba huo.
إرسال تعليق