MWANAFUNZI wa darasa la nne shule ya msingi Mji Mpya aliyetambuliwa kwa jina la Doris Samwel (10) amekutwa amekufa ndani ya karo la maji. Maiti ya mwanafunzi huyo ilikutwa jana saa 2:00 asubuhi maeneo ya Majohe Viwege, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Marietha Minangi, alisema maiti hiyo ilikutwa ndani ya karo la maji jirani na nyumba yao.
Inasadikiwa mtoto huyo alitumbukia wakati akijaribu kuchota maji.
Katika tukio jingine, watu wawili wamekufa papo hapo baada ya pikipiki yao kugongana na lori, wilaya ya Temeke.
Ajali
hiyo ilitokea juzi saa 2:00 usiku katika Barabara ya Yombo Buza eneo la
Mama Kibonge, ambapo gari aina ya Mitsubishi Rosa yenye namba T166 BXN
ikiendeshwa na mtu asiyefahamika akitoka Tandika kwenda Buza, alipofika
maeneo hayo aligongana na pikipiki yenye namba T849 CSE aina ya Boxer.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema, katika ajali hiyo
mwendesha pikipiki na abiria wake waliotambuliwa kwa majina ya Ismaili
Hamidu (35) na Twaha Jordan (30) walikufa.
Katika
tukio la tatu, mtembea kwa miguu ambaye hajafahamika amekufa baada ya
kugongwa na gari akivuka barabara ya Obama eneo la Taasisi ya Magonjwa
ya Saratani ya Hospitali ya Ocean Road.
RC aigiza
polisi kukamata gari za Serikali Na Khatib Suleiman, Zanzibar POLISI
Zanzibar imetakiwa kuzichukulia hatua za kisheria gari zote za Serikali
ambazo zitabainika kuendeshwa bila ya kukatiwa Bima.
Agizo
hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdalla Mwinyi
mwishoni mwa wiki, wakati alipofungua semina ya siku moja ya Shirika la
Bima kwa Jeshi la Polisi la usalama barabarani mjini hapa.
Alisema
ni makosa gari za Serikali kuendeshwa bila ya kukatiwa bima kwani agizo
la Serikali linazitaka gari hizo kukatiwa bima kama zilivyo gari
nyingine za abiria.
Aidha
aliwataka askari wa barabarani kupambana na mbinu mbalimbali
zinazofanywa na madereva ambao baadhi yao huonesha kadi za bima bandia
na kulikosesha taifa mapato.
Mapema
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Bima, Nasir Ahmed Abrahman, alisema
Shirika la Bima limejizatiti kuhakikisha linaongeza mapato yake kwa
kubuni njia mbali mbali katika vianzio vipya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Mkadam Khamis Mkadam, alisema Polisi
imejipanga kuhakikisha inapambana na baadhi ya watu wajanja wenye nia ya
kulikosesha shirika mapato kwa kufanya udanyanyifu.
CHANZO:HABARILEO
Post a Comment