

Waombolezaji
wakisubiri kuuaga mwili wa marehemu Anastazia Lackford Magafu
aliyefariki baada ya kudaiwa kuchomwa moto na baba yake kisha kupewa
juisi yenye sumu.

Mwili wa Anastazia Lackford Magafu wakati ukiagwa katika Shule ya Sekondari Mwanza.
Mwili wa marehemu Anastazia Lackford Magafu juzi uliagwa katika Shule ya Sekondari Mwanza alipokuwa akisoma enzi za uhai wake.
Inadaiwa
kuwa kifo cha marehemu Anastazia kimesababishwa na sumu iliyowekwa
kwenye juisi aliyopelekewa na baba yake, Lackford Magafu maarufu kwa
jina la DJ Lackford, wakati akiwa amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya
Bugando (BMC) akitibiwa majereha ya moto.
Tukio
la kifo hicho liliotokea Aprili 16 mwaka huu, ikiwa ni muda mfupi baada
ya kunywa juisi inayodaiwa kuwa na sumu, hivyo kuzua utata wa chanzo
cha kifo hicho.
>>>GPL
إرسال تعليق