![]() Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Prosper Msofe (kushoto) ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Daraja Mbili kupitia CHADEMA na Diwani wa Kata ya Levolosi, Ephata Nanyaro nae kupitia Chadema, wakisubiri kupata matibabu baada ya kupata kipigo kutoka kwa mgambo wa Jiji la Arusha leo wakati wakiwatetea Wamachinga.Kwa mujibu wa Diwani Nanyaro, anasimulia kwamba leo asubuhi alipata taarifa kuwa mgambo wa Jiji wanawapiga wananchi wafanyabiashara ndogondogo na kupora mali zao maeneo ya Kata yake, ndipo akaelekea kukutana na Naibu Meya kujionea hali halisi. Anasema alipofika alijaribu kuwasihi mgambo hao kuwa sio utaratibu kuwapiga wananchi maana hata taratibu za ukamataji haziruhusu kupiga raia. |

Post a Comment