Nameless, Radio, Weasel, Jaguar, STL, Navio, Bebe Cool na wengine Kwenye Reality TV Show “Tusker Twende Kazi”, Nairobi to London

STL
“Tusker Twende Kazi” ni Reality TV show ambayo imewakutanisha mastaa wengi sana kwenye nyanja tofauti za michezo nchini KENYA, UGANDA na TANZANIA. Reality show hii ambayo inarushwa hivi sasa kupitia kituo cha television cha nchini Kenya CITIZEN TV na vituo mbali mbali vya television Kati nchi za East Africa, ambayo inaonyesha safari ya wananchi 50 kutoka Africa Mashariki wakiwemo Nameless, Radio, Weasel, Jaguar, STL, Navio, Bebe Cool na wengine wengi ambao watafanya Safari kutoka nchini KENYA mpaka kufika LONDON ndani ya siku 50, kumpelekea chupa ya TUSKER LAGER mchezaji wa RUGBY ndugu HUMPHREY KHAYANGE ambae ni raia wa KENYA aishie mjini LONDON.
HumphreyKayange
Washiriki hao walijiunga katika Timu ya watu wawili wawili, ambao itajumuisha Mwananchi wa kawaida kutoka East Africa na Celebrity. Safari hii itakuwa na Wakenya 14 ambao ni wanamichezo (Sports) na wanamuziki (Musicians) pamoja na wananchi wa kawaida kutoka Kenya 14 na wengine kutoka Uganda na Tanzania ambao wamechaguliwa. Matayarisho ya kipindi hiki yalianza tarehe 12 Dec 2013 na safari ya kwenda London ilianza February ambayo inachukua siku 50 za safari ambapo washiriki hawa watapita nchi 13 katika mabara mawili ya dunia.
STL
PICHA JUU: STL ambae yupo kwenye kundi TEAM 24, ametuma picha kwenye mtandao wa twitter kuwa TEAM 24 tayari wameshaingia mjini PARIS tayari kumalizia ngwe yao iliyobaki, ambapo saa moja lililopita NAVIO ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa twitter akisema………….  ”Tomorrow I’m heading off to the UK. Send me your shopping list! #TwendeKazi #NoHoldingBACK

Post a Comment

Previous Post Next Post