Google Video
Waweza kutumia huduma maalum ya kusearch video kwa Google, cheki picha hapo chini hatua kwa hatua. Bofya hapa kwenda Google Video. Ukiwa mwanzo wa Google Video andika chaguo lako unalotafuta kisha bofya enter.
Hakikisha unacheki sehemu ya Search Tools, kisha utaona hizo sehemu za machaguzi. Utaona uchaguzi hizi angalia sehemu ya Any duration, kisha chagua Long (20+min) yaani movies za zaidi ya dakika 20.
Hulu
Kuna website inayoitwa jina la HULU, hata hivyo kuitembelea ni lazima uwe upo Marekani.
Hata hivyo kuna AddOn unayoweza kuinstall kwa kompyuta yako
itakuwezesha kufungua program hiyo website ya HULU hata kama upo
Tanzania.
AddOn inaitwa HOLA, na utaipata kwa kubofya hapa Kama unatumia GOOGLE CHROME
Utakapokuwa umeinstall hiyo Hola utaweza kujiandikisha kuitumia
kisha utabofya juu kwenye alama ya hilo Hola ambapo itakuwa juu karibu
na sehemu ambapo anuani za website huonekana -upande wa kulia wa
kompyuta yako.
Hola itakuonyesha websites ambazo utaweza kuzitembelea hata ukiwa
Tanzania. Hata hivyo katika makala hii napendekeza ubofye HULU ili
ujionee movies bure kabisa.
Post a Comment