Namna ya kubadili kitu unachopenda na kukifanya kuwa taaluma yako.

woman-computer
 
Je unatumia muda mwingi kila siku kufanya kitu usichokipenda? Je unafanya kazi ambayo inaonekana kukuboa? Je unahisi hauishi maisha unayostahili kwa sababu ya kile unachakifanya? Haya ni maisha yako yanakwisha kila dakika na kila wakati. Usikate tamaa, kuna uwezekano wa wewe kutumia siku nzima kufanya kile unachopenda kukifanya. Hebu tazama vitu hivi  vitano vinavyoweza kukusaidia kubadili kitu unachopenda kukifanya kila siku kuwa taaluma.

1. Hakikisha unatumia maisha yako yote kukifanya.  

Kwasababu unafikiri kubadilisha kitu unachokipenda kuwa taaluma, hapa ninaangalia kitu ambacho unakijua na umekuwa ukikifanya tu kwa mambo yako binafsi. Kitu cha msingi unahitaji kujiuliza wewe mwenyewe je una uhakika unataka kufanya hicho? Kama unafikiria kubadilisha kitu cha kawaida ulichozoea kukifanya kuwa taaluma, si kwamba hautafanya kazi sana utakuwa unajidanganya. Kama kazi zote huwa zinachanganya wakati fulani, hivyo tegemea jambo kama hilo kutokea, itafika mahali utaboreka. Hivyo ujue majukumu yako yatakavyokuwa unapobadilisha kuwa taaluma, na kama una ujasiri endelea mbele.

2. Fanya Utafiti

Unapotaka kubadilisha kitu chochote unachokifanya kuwa ndio taaluma yako fanya utafiti wa kina, ili ujue hilo jambo na wazo lako linawezekaneje kibiashara? Tafuta kujua unahitaji nini kukamilisha huo mradi, mtaji unaohitajika, Uendeshaji wake, sheria za kodi n.k. Vile vile fanya utafiti wa kampuni unayotaka kufungua na ni nini kinahitajika, au aina ya biashara na kitu kinachohitajika. Tafuta kujua watu wanaofanya kazi kwenye nyadhifa  hizo wana elimu kiasi gani au wana elimu hasa inayohusu nini? Katika kuendesha biashara hiyo, kama huna vigezo unafanyaje?

3. Kutana na watu wenye uzoefu

Jaribu kukutana na watu wenye uzoefu na kile unachotaka kufanya, usiache kutengeneza mtandao wa watu kwenye matukio mbalimbali. Unapokua na mtandao ni rahisi kutangaza biashara yako na kupata fulsa mpya ambazo ulikua huna.

4. Tafuta taaluma inayoelekeana

Kubadilisha kitu unachafanya kawaida kuwa taaluma inahitaji kujitoa muhanga, ni sawa sawa na kutengeneza juisi ya ndimu na iwe na mvuto. Utahitaji kufanya vitu vingi ambavyo vitakusaidia kujijenga na kuweza kufikia malengo fulani hata kwa kujitolea na kufanya kazi na mashirika yanayofanya kile ambacho unafikiri kukifanya ili uweze kujifunza zaidi kabla ya kuanza cha kwako.

5. Anza kufanya kwa muda wa ziada kwanza

Kabla ya kuanza hicho kitu kwa kasi, anza kidogo kidogo. Kama ni Jumamosi na Jumapili siku ambazo hauendi kazini uanze kukiweka katika matendo au baada ya masaa ya kazi. Kwanini uanze kidogo kidogo? Kwakuwa bado hujajua soko litatoa mwitikio gani, hivyo lazima uanze kwa kujaribu kabla ya kuingia mzima mzima. Unapoendelea kufanya hivyo ndipo utajua nini kinafanyika na gharama ya kuingia huko ni nini na wewe uchukue hatua gani za mapema. Fanya kwa umakini na taratibu, Je uko tayari kuchukua hatua?

Post a Comment

Previous Post Next Post