Je unatumia muda
mwingi kila siku kufanya kitu usichokipenda? Je unafanya kazi ambayo
inaonekana kukuboa? Je unahisi hauishi maisha unayostahili kwa sababu ya
kile unachakifanya? Haya ni maisha yako yanakwisha kila dakika na kila
wakati. Usikate tamaa, kuna uwezekano wa wewe kutumia siku nzima kufanya
kile unachopenda kukifanya. Hebu tazama vitu hivi vitano vinavyoweza
kukusaidia kubadili kitu unachopenda kukifanya kila siku kuwa taaluma.
1. Hakikisha unatumia maisha yako yote kukifanya.
Kwasababu
unafikiri kubadilisha kitu unachokipenda kuwa taaluma, hapa ninaangalia
kitu ambacho unakijua na umekuwa ukikifanya tu kwa mambo yako binafsi.
Kitu cha msingi unahitaji kujiuliza wewe mwenyewe je una uhakika unataka
kufanya hicho? Kama unafikiria kubadilisha kitu cha kawaida ulichozoea
kukifanya kuwa taaluma, si kwamba hautafanya kazi sana utakuwa
unajidanganya. Kama kazi zote huwa zinachanganya wakati fulani, hivyo
tegemea jambo kama hilo kutokea, itafika mahali utaboreka. Hivyo ujue
majukumu yako yatakavyokuwa unapobadilisha kuwa taaluma, na kama una
ujasiri endelea mbele.
2. Fanya Utafiti
Unapotaka
kubadilisha kitu chochote unachokifanya kuwa ndio taaluma yako fanya
utafiti wa kina, ili ujue hilo jambo na wazo lako linawezekaneje
kibiashara? Tafuta kujua unahitaji nini kukamilisha huo mradi, mtaji
unaohitajika, Uendeshaji wake, sheria za kodi n.k. Vile vile fanya
utafiti wa kampuni unayotaka kufungua na ni nini kinahitajika, au aina
ya biashara na kitu kinachohitajika. Tafuta kujua watu wanaofanya kazi
kwenye nyadhifa hizo wana elimu kiasi gani au wana elimu hasa inayohusu
nini? Katika kuendesha biashara hiyo, kama huna vigezo unafanyaje?
3. Kutana na watu wenye uzoefu
Jaribu kukutana
na watu wenye uzoefu na kile unachotaka kufanya, usiache kutengeneza
mtandao wa watu kwenye matukio mbalimbali. Unapokua na mtandao ni rahisi
kutangaza biashara yako na kupata fulsa mpya ambazo ulikua huna.
4. Tafuta taaluma inayoelekeana
Kubadilisha kitu
unachafanya kawaida kuwa taaluma inahitaji kujitoa muhanga, ni sawa
sawa na kutengeneza juisi ya ndimu na iwe na mvuto. Utahitaji kufanya
vitu vingi ambavyo vitakusaidia kujijenga na kuweza kufikia malengo
fulani hata kwa kujitolea na kufanya kazi na mashirika yanayofanya kile
ambacho unafikiri kukifanya ili uweze kujifunza zaidi kabla ya kuanza
cha kwako.
5. Anza kufanya kwa muda wa ziada kwanza
Kabla ya kuanza
hicho kitu kwa kasi, anza kidogo kidogo. Kama ni Jumamosi na Jumapili
siku ambazo hauendi kazini uanze kukiweka katika matendo au baada ya
masaa ya kazi. Kwanini uanze kidogo kidogo? Kwakuwa bado hujajua soko
litatoa mwitikio gani, hivyo lazima uanze kwa kujaribu kabla ya kuingia
mzima mzima. Unapoendelea kufanya hivyo ndipo utajua nini kinafanyika na
gharama ya kuingia huko ni nini na wewe uchukue hatua gani za mapema.
Fanya kwa umakini na taratibu, Je uko tayari kuchukua hatua?
إرسال تعليق