Taarifa hii imethibitishwa na meneja wa Azam fc, wana Lambalamba, Jemedari Said.
“Kavumbagu
has done a deal! Tumemalizana nae na amesaini rasmi mkataba wa mwaka
mmoja, so tutakuwa nae msimu ujao kwenye kampeni ya kutetea ubingwa wetu
pamoja na michuano ya klabu bingwa ya Afrika,” alifunguka Jemedari.
Mshambuliaji
huyo hatari na nahodha wa timu ya Taifa ya Burundi ameamua kumwaga wino
Azam baada ya Uongozi wa Yanga kusuasua kumpa mkataba mwingine baada ya
ule wa miaka miwili kumalizika.
Kavumbagu
mara kadhaa alikaririwa na vyombo vya habari kuhitaji mkataba mpya
katika klabu ya Yanga, lakini viongozi wa kalbu hiyo hawakuonesha nia na
leo hii imeamua kuanza maisha mapya Chamazi.
Katika
maelezo yake, Kavumbagu alieleza kuwa mpira ni sehemu ya maisha yake na
kazi yake, hivyo yuko tayari kuichezea klabu yoyote yenye nia ya
kumsajili kwa masharti ya kukidhi mahitaji yake ya msingi.
Azam fc
wenye nia ya kufanya vizuri katika michuano ya ligi ya mabingwa barani
Afrika mwakani, wamekusudia kuongeza nguvu katika kikosi chao.
Kocha mkuu, Mcameroon, Joseph Marius
Omog ameenda likizo kwao Cameroon , lakini uongozi wa Azam ulithibitisha
kupokea taarifa ya mapendekezo yake na tathimini ya msimu uliomalizika
aprili 19 mwaka huu.
Usajili huu unathibitisha kuwa Kavumbagu alikuwa katika rada za Omog na aliwaachia viongozi mpango mzima.
Kuzugazuga
kwa Uongozi wa Yanga kumemfanya nyota huyo kuangukia mikononi mwa
matajiri wa Azam fc japokuwa alikuwa tayari kumwaga wino tena katika
klabu ya Yanga.
Mkataba aliosaini Azam fc unasemekana kuwa na masilahi bora zaidi ya ule wa Yanga. Nyota huyo mwenye uchu wa mabao alijiunga na Yanga mwaka 2013 akitokea klabu ya Atletico ya nchini Burundi.
Kavumbagu
amesaini mbele ya Katibu Mkuu wa klabu ya Azam, Nassor Idrisa makao
makuu ya klabu, Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Nassor
amekaiririwa na Tovuti ya klabu akisema; “Tumepata mshambuliaji mzuri,
ambaye tayari ana uzoefu wa kucheza Ligi Kuu ya Tanzania kwa misimu
miwili, mchezaji huyu ni chaguo la kocha wetu Joseph Omog, ambaye
alivutiwa naye baada ya kumuona akichezea klabu yake zamani, Yanga
SC,”alisema.
Kwa
upande wake, Kavumbangu ameiambia Tovuti ya Azam kuwa; “Mimi ni
mchezaji, kazi yangu ni mpira. Nimemaliza mkataba Yanga, lakini viongozi
hawaniambii kitu, nimepata ofa nzuri Azam nikaamua kusaini,”.
Mshambuliaji
huyo mrefu mwenye nguvu amesema sasa akili yake anaipeleka kwa mwajiri
wake mpya, Azam FC ambako pia amepania kwenda kushinda mataji na
kuiwezesha timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na
familia yake kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika.
“Mimi
sasa ni mchezaji wa Azam, nafurahi kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida
yangu huwa nashabikia klabu nayochezea, sasa mimi ni mshabiki namba moja
wa Azam,”amesema.
Kavumbangu
alitua Yanga mwaka 2013 akitokea Atletico ya Burundi na katika mechi
misimu miwili ya kuichezea klabu hiyo, amefunga mabao 31 katika mechi 63
za mashindano yote, moja tu la penalti. Kila la heri Kavumbagu katika maisha mapya Azam fc.
إرسال تعليق