
Mahad aliwasiliana na ‘Live Nation’ ambao ni joint venture na kampuni ya msanii huyo ‘Rock-A-Fella Records’ alisema atapiga mnada mzigo huo au alipwe kiasi cha dola za kimarekani laki moja ($100,000) kwa ajili ya kuhifadhi mzigo kwa muda wote huo. Walikubaliana kumalizana kwa $75,000 na kukubaliana kukutana mitaa ya North-ridge California, kwa malipo hayo na ili kuweza kukabidhiana mizigo hiyo bila kujua kuwa kampuni hiyo ya Jay Z walikuwa wameshawasiliana na Polisi ambao walimtia hatiani na kuzuia mzigo huo mpaka siku ya Mahakama ambapo Judge atakapoamua nani akabidhiwe mali hiyo.
إرسال تعليق