‘Ni kama nilimtabiria’, Izzo Bizness auzungumzia ushindi wa ‘Riz-One’ (Audio).

izzo
 

Ombi la Izzo Bizness kwa mtoto mkubwa wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani la kumwambia ‘mshua’ wake maisha yalivyo magumu kwa wananchi wa Tanzania na hivyo alifanyie kazi, limepata urahisi kwakuwa ‘Riz One’ ameshinda uchaguzi wa jimbo la Chalinze.

Ridhiwani Kikwete, mbunge mteule wa Chalinze

Hiyo ina maana kuwa akiwa kama mbunge, kwa sasa atakuwa na mamlaka ya kuwasilisha moja kwa moja malalamiko ya watu kama Izzo B, kupitia chombo hicho kinachotunga sheria za nchi.
“Nafikiri yeye mwenyewe pia ana sababu kubwa sana za kunishukuru,” Izzo B ameiambia Bongo5 kuhusiana na alivyojisikia baada ya Ridhiwani kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo mdogo uliofanyika jana.
Izzo anaamini kuwa kwenye wimbo huo ni kama alimtabiria Ridhiwani. “Mimi mwanzoni wakati nimeimba ‘Ongea na Mshua’ ilikuwa kwamba yeye aende amwambia mzee, lakini sasa imekuja kuwa kweli ameingia bungeni. Imekuwa kama TALAWANDA 1 (5)imerahisishwa zaidi sababu nikisema ongea na mshua inakuwa ina make sense zaidi.”
Izzo amesema kuwa tangu atoe wimbo huo zaidi ya miaka miwili iliyopita amekuwa akiwasiliana na mbunge huyo mteule na wakati ameanza kampeni ya uchaguzi alimuomba akamsaidie kwenye kampeni hizo.
“Kuna vitu vidogo tu ambavyo tulipishana, niliangalia pia katika upande wangu. Kilikuwa sio kitu cha kusaidiana kimasihala kwakuwa unapoamua kuingia kwenye kampeni kumsaidia mtu ujue ushaamua kutake risk. Na hapo mimi nilikuwa naenda kukipa tafu chama cha CCM lakini mimi natokea jimbo ambalo limeshikiliwa na CHADEMA na wananchi asilimia kuwa ni CHADEMA.”
Msikilize zaidi hapa.


Post a Comment

أحدث أقدم