
Imetaarifiwa
kuwa jumla ya watu 105 wameisha stowaway na ni 25 tu ndio walionusurika
na hii ni kutokana na baridi kali na ukosefu wa oxygen ndege inapokua
angani.
Mtoto wa
miaka 16 aliyetoroka na ndege kwa kujificha kwenye milango ya kukunjia
matairi ya ndege inapokuwa angani anaendelea vizuri na amewekwa kwenye
hifadhi ya watoto na mamlaka husika bado haijamfungulia mashtaka kwa
madai kwamba kunusurika kifo wakati akiwa angani ni mateso tosha na
wanashangaa jinsi gani alivyopenya uzio wa uwanja wa ndege wa California
na kufanikiwa kudandia ndege hiyo na kuwa angani kwa saa 5 mpaka
Hawaii.
إرسال تعليق