![]() |
| Mmoja wa wasichana watakaonekana kwenye video hiyo |
Rapper Nikki wa Pili wa kampuni ya Weusi amesema changamoto
waliyokuwa nayo baada ya kuachia video ya ‘Nje ya Box’ ni kutengeneza
video inayofuata itakayokuwa kali zaidi kuliko hiyo.. na hilo
wamefanikiwa kulifanya kwa kushoot video ya ‘Gere’ nchini Kenya.
“Gere tumeshafanya na imeipiku ‘Nje ya Box’ katika misingi ya
creativity, quality na namna picha inavyoonekana,” Nikki wa Pili
ameiambia Power Jams ya East Africa Radi. “Halafu pia tumekuja na taste
mpya unajua Nisher ni bora ana taste yake na Inos ni bora ana taste
yake, ukiangalia video ya Jaguar, Octopizzo. Kwahiyo tumefanya video
kali sana. Tunategemea impact itakuwa kubwa kwasababu video ni kali.”

إرسال تعليق