NMB yafungua tawili jipya Kigoma

Benki ya NMB imezindua rasmi tawi lake jipya mjini Kigoma. Uzinduzi wa tawi hilo lililoko katika jengo la Bima barabara ya Lumumba katika jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ulifanyika mwishoni mwa wiki. Aidha, tawi hilo lililo mkabala na Soko Kuu la Kigoma, limelenga kutoa huduma kwa watu binafsi na wakazi wengi wa maeneo hayo hususan wafanya biashara ndogo ndogo.
DSC_0935 Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw. Ramadhani Maneno akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Kigoma .Hafla hii ya uzinduzi ilifanyika katika viwanja vya tawi la NMB Kigoma.Wakishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Bw. Abraham Augustino (kushoto) pamoja na Meneja wa tawi la NMB Kigoma, Bw. Rogers Malang’u
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw.Ramadhani Maneno alisema tawi hilo litasaidia kusogeza karibu huduma za kifedha kwa wakazi wa Kigoma kutokana na mkoa huo sasa kupata maendeleo ya kiuchumu na kijamii.“Binafsi naishukuru NMB kwa juhudi zake za kuboresha huduma zake kwa lengo la kukidhi matakwa ya wateja na kuwafikia katika maeneo mbalimbali chini,” alisema Maneno.
DSC_0967 Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw. Ramadhani Maneno akipata maelezo kuhusu huduma za ‘NMB Fast Track’ kutoka na Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Bw. Abraham Augustino (kushoto) pamoja na Meneja wa tawi la NMB Kigoma, Bw. Rogers Malang’u
Kwa upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Bw. Abraham Augustine alisema,”Tumekuwa tukifanya jitihada za kuhakikishia kwamba benki hii inatoa huduma bora kwa wateja wetu wengi. Katika juhudi hizi, tumekuwa tukipanua mtandao wa matawi kuhakikisha kwamba tupo katika maeneo jirani na wateja wetu.”
DSC_0969
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Bw. Charles Gichilu (kulia) akipata huduma kutoka benki ya NMB. Pembeni yake ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw. Ramadhani Maneno
DSC_0891
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo

Post a Comment

أحدث أقدم