![]() |
Waumini wa kanisa katoliki wakifuatilia sherehe za kutangazwa watakatifu mapapa John XXIII na John Paul II |
Mapapa wa zamani, John XXIII na John Paul II wametangazwa
watakatifu Jumapili hii na Papa Francis hafla iliyoshuhudiwa na umati
mkubwa wa waumini wa kanisa katoliki kwenye viwanja vya St. Peter’s
Square, jijini Vatican.
Mamilioni ya watu wengine duniani wameangalia kupitia runinga tukio
hilo la viongozi wa zamani wa kanisa katoliki wakipewa utakatifu.
Vatican ilitarajia watu milioni 1 kukusanyika kwenye kanisa hilo
pamoja na barabara za kuelekea kwenye kanisa la St. Peter’s Basilica.
Sherehe hizo zimehudhuriwa na makadinali 150, maaskofu 1,000 na mapadre
6,000. Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 100 nao wamehudhuria wakiwemo
marais 24.

Rais Robert Mugabe na familia yake
Tukio hilo ni kubwa zaidi jijini Vatican tangu kuchaguliwa kwa Papa Francis mwaka jana.
Hizi ni baadhi ya picha.

Papa Emeritus Benedict XVI, aliyejiuzulu mwaka jana kwa sababu
za kiafya alialikwa na Papa Francis lakini hakuwepo kwenye madhabahu





إرسال تعليق