![]() |
Peter na mkewe Lola |
Paul anayetumia @rudeboypsquare kwenye Twitter ameandika: PSQUARE! Stronger than Ever!!! na Peter anayetumia jina @PeterPsquare akiandika: FOREVER PSQUARE!
Awali, Peter alidaiwa kugoma kuondoa kinyongo chake kwa kaka zake akiwemo Paul licha ya kuombwa sana marafiki zake.
Pacha huyo alisema kama familia inataka kuwa na amani ni lazima imkubali na kumheshimu mke wake Lola. “Peter amechoka kutokana na kutumia miaka mingi kuiomba familia yake imkubali mwanamke aliyeamua kumuoa. Anataka Lola akubalike kwenye familia kama Anita (mke wa Paul) alivyokubalika bila kuzingatia utofauti wa umri wao,” chanzo kilicho karibu na familia hiyo kililiambia gazeti Vanguard.

Vyanzo vilisema kuwa ugomvi wao ulikuwa mkubwa zaidi baada ya kubainika kuwa Peter amemnunulia nyumba Lola nchini Marekani.
Vanguard limedai kuwa kwa sasa Paul na Peter wameanza kuongea tena japo Paul hajaonesha kukubali ombi la pacha wake kwakuwa hata mama yao kabla hajafa alikuwa hajakubali uhusiano wa Peter na Lola.
Katika hatua nyingine Kaka yao Jude Okoye ambaye anadaiwa kuwa na mchango mkubwa wa ugomvi wa Peter na Paul, alitweet kueleza kuwa kwake familia ni kitu cha kwanza na kwamba P-Square itadumu.
Sababu za ugomvi baina ya mapacha wa P-Square zafahamika
Alhamis hii alitweet:
Family is everything indeed. Long live PSQUARE!
— IG: @Judeengees (@judeengees) April 25, 2014
إرسال تعليق