Emmanuel Okwi.
KOCHA
Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amesema mchezaji Emmanuel Okwi
hayupo kambini na suala lake lipo juu ya uwezo wake na hawezi kumtumia
kwenye mechi ya leo dhidi ya Kagera Sugar.
Pluijm amesema mbali na Okwi, kuna wachezaji wengine kadhaa hawapo, lakini yeye anaendelea kupambana na wale waliopo.
Akizungumza na Championi Jumatano, kocha huyo
alisema sababu za baadhi ya wachezaji wake kutokuwepo kama Okwi zipo juu
ya uwezo wake, hivyo hawezi kuzungumza lolote kuhusiana na wachezaji
hao lakini kwenye kikosi chake leo hawawezi kucheza.
Pluijm alisema kuwa ataendelea kuwatumia wachezaji wake haohao
waliopo kambini na si vinginevyo kwa sababu hao ndiyo wanaofanya mazoezi
na siyo ambao wapo nje ya kambi.
“Suala la mshambuliaji Emmanuel
Okwi kutokuwepo kambini sijui ni kwa nini, sababu zipo juu ya uwezo
wangu, siwezi nikasema vitu ambavyo sivifahamu.
Wakati huohuo, daktari wa timu hiyo, Juma
Sufiani, alisema kuwa, kwa sasa kikosi hicho kina wachezaji wagonjwa
wawili ambao ni Haruna Niyonzima na David Luhende ambao walikuwa
wanasumbulia na malaria lakini afya zao zimeanza kuimarika kwa kiasi
kikubwa.
“Haruna Niyonzima na Luhende ndiyo wagonjwa lakini
wanaendelea vizuri na wameanza mazoezi mepesi binafsi kisha wataungana
na timu,” alisema Juma.
Post a Comment