Rais Jakaya Kikwete na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein jana wamewaongoza mamia ya wananchi
katika dua maalum ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi marehemu Abeid Amani Karume.
Karume aliuawa April 7 mwaka 1972 akiwa katika jengo lililokuwa Makao
Makuu ya Chama cha Afro Shirazi huko Kisiwandui mjini Unguja wakati huo
ambalo sasa ni Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi- Zanzibar.
Viongozi wengine waliohudhuria dua hiyo ni pamoja na Makamu wa Rais
Dk. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Zanzibar
Awamu ya Sita Dk. Amani Abeid Amani Karume.
Katika kiwanja cha Ofisi Kuu ya CCM dua zilisomwa na viongozi wa
madhehebu mbalimbali ya dini na baadae viongozi pamoja na watu wengine
walioteuliwa walikwenda kwenye kaburi la marehemu ambako waliweka
mashada ya maua
إرسال تعليق