
Juhudi za uokozi zingali zinaendelea
Rais wa Korea kusini Park Geun
Hye amemkosoa nahodha na wafanyikazi wa Feri ya abiria iliozama kwa
kuikimbia feri hiyo na hivyobasi kufananisha vitendo vyao na mauaji.
Matamshi ya rais Park yanafuatia uchapishaji wa
mawasiliano kati ya feri hiyo na waokozi ,yaliobaini kwamba kulikuwa na
hali ya wasiwasi mbali na kutokuwepo mpangilio wa uokozi.Wapiga mbizi wanaendelea na juhudi za kutafuta mili ya watu waliozama na feri hiyo huku wakijitahidi kuingia ndani ya feri yenyewe.
Habari zilizotangazwa kuhusu mawasiliano ya mwisho kati ya wafanyakazi wa Feri iliyozama Korea Kusini na maafisa wa kudumisha usalama baharini zinaonyesha kuwa kulitokea hali ya wasiwasi kabla ya mkasa huo, ambayo huenda ilichangia pakubwa vifo vya abiria wengi katika feri hiyo.
Taarifa hiyo mpya ilitolewa Jumapili alasiri wakati ambapo imethibitishwa kuwa maiti 62 zimepatikana kwenye mabaki ya feri hiyo, na kufanya idadi ya watu waliothibitishwa kufariki kufikia 58. Zaidi ya watu 240 hawajulikani waliko hivi sasa.

Jamaa wa waathiriwa walikabiliana na polisi wakilaumu waokozi kwa kujikokota
Mama mmoja alisema kuwa watoto waliofariki walikuwa wakitunzwa vizuri.
"Naamini watoto hao wako mbinguni ," mama huyo alisema.
Jung Maria, mwanamke aliyejitolea kuzisaidia familia za walioathirika, alisema kuwa jamaa za watu wasiojulikana waliko wanapaswa kusikia kilichotokea kwa njia moja au nyingine.
"ikiwa wamefariki, tunapaswa kupata miili yao haraka iwezekanavyo. Na iwapo kutatokea muujiza basi turejeshewe watoto hao upesi pia, alisema mfanyakazi huyo wa kujitolea
Idadi kubwa ya abiria katika meli hiyo walikuwa wanafunzi wa shule ya upili waliokuwa wakienda kwenye mojawapo wa kisiwa kubarizi. Hadi kufikia sasa kumekuwa kungali kuna ubishi mkubwa iwapo nahodha mwenyewe alikuwa ameshikilia sukani.
إرسال تعليق