Ratiba ya mazishi ya Maalim Gurumo

20140414-094534.jpg
Ratiba hii ya mazishi ya Gwiji la muziki wa Dansi hapa nchini ambae amegariki dunia siku ya jana, leo imetolewa na mtoto wa marehemu Gurumo leo asubuhi. Ratiba ya mazishi ya marehemu Gurumo itakua kama ifuatavyo
-LEO saa 10 jioni kutakuwa na kisomo nyumbani kwa marehemu Tabata-Kisukulu jijini Dar es Salaam.
-Kesho saa 3 asubuhi mwili wa marehemu utawasili nyumbani kwake kwa ajili ya sala.

-Saa 4 asubuhi safari ya kuelekea kijiji cha Masaki wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani kwa maziko.
MUNGU Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi, Amina

Post a Comment

أحدث أقدم