
Subira ya mashabiki wa Ray C inaelekea ukingoni huku hamu ya kusikia sauti yake tena ikiongezeka kila anapo-tease ujio wake.
Jana, Ray C amepost kwenye Instagram picha ambazo zinaonekana kuwa ni
maalum kwa ajili ya utambulisho wa ujio wa kazi zake huku maandishi
yake kwenye post moja yakiashiria huenda picha hizo zikawa ni sehemu ya
video ya wimbo wake.
“Behind the seen @albertmanifester kazi imeanza mashallah sauti tamu
itaanza kusikika soon!!!!!!!Thank you lord.” Ameandika Ray C.
“Work!work it girl!!!!kazi mpk weekend!kimya kimya kazi ndo ishaanza
jiandaeni wapenzi!” Ameandika kwenye post nyingine ya upigaji picha
ambao umefanywa na Albet Manifester.
Katika hatua nyingine, Mwimbaji huyo ameendelea kupost logo
mbalimbali za ‘Ray C Foundation’ akiwaomba ushauri mashabiki wake ipi
itumike.
>>Times 100.5 fm
إرسال تعليق