Na Riziki Mashaka.
Mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory
Coast ambaye pia anaichezea klabu ya Manchester City, Yaya Toure amesema
kuwa asili yake ya uafrika ni kigezo kikubwa kinacho mfanya ashindwe
kupata tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Toure alisema kuwa mashabiki
wengi wa ulaya hususan ni uingereza hawamthamini sana kwa kuwa ni
muafrika.
Akiongea na City Tv, Toure alisema
''ukija Afrika ukiuliza jina Messi kila mtu atakwambia anamjua lakini
ukienda ulaya na kuuliza jina Yaya Toure watu watakuuliza, Yaya Toure ni
nani? Hali hii inaonesha kuwepo kwa ubaguzi wa hali ya juu katika soka
la ualaya, alisema Yaya.
Baada ya kunyakua kombe cha Capital
One katika dimba la Wembley mnamo mwezi Machi, mchezaji Samir Nasri
ambaye pia ni kiungo wa Manchester City alisema ''Yaya Toure ni mchezaji
ambaye anastahili kuwa kiungo bora wa dunia kama asingekuwa muafrika''
kauli hiyo ya Nasri iliungwa mkono na kiungo huyo raia wa Ivory Coast ''
nafikiri alichokisema Nasri ni kweli kabisa'' Yaya Toure aliwaambia
waandishi wa habari wa bbc.
Yaya Toure ni mmoja kati ya wachezaji
sita waliochaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka katika soka
la Uingereza maarufu kama '' Professional Footballers' Association
(PFA)'' ambapo atashindana na miamba mingine kama Steven Gerrard, Daniel
Sturridge and Luis Suarez, Eden Hazard and Adam Lallana na mshindi wa
tuzo hiyo atatangazwa Aprili 27.
Toure amewahi kushinda vikombe vya
ligi akiwa Uispaniola, Uingereza na Ugiriki pia aliwahi kunyakua kombe
la mabingwa ulaya akiwa na Barcelona.
إرسال تعليق