Msanii wa filamu na muziki nchini, Snura Mushi amelazwa katika
hospitali moja iliyoopo eneo la Kinondoni kutokana na matatizo ya presha
ambayo yameanza kumsumbua tangu jana usiku.
Akizungumza na 255 ndani ya XXL ya Clouds FM, meneja wa Snura,HK
amesema kuwa Snura bado yupo hospitali baada ya kuzidiwa tena leo
asubuhi.
“Ni kweli toka jana usiku manake toka last week, alikuwa kwenye
show amerudi vizuri,lakini tangu jana usiku amezidiwa kama saa nne nane
saa tisa,usiku sana nikapigiwa simu, yeye anaishi around maeneo ya
komakoma hapo na mimi naishi around mitaa ya studio,kwahiyo kama hatua
kumi na mbili to ishirini na nne hivi nimefika kwake, nikamchukua
nikampeleka hospitali amerudi, lakini sasa hivi tena kidogo hali
imeharibika tena kwahiyo tumemrudisha tena hospitalo amelazwa. Ni
masuala ya presha kwa mujibu wa daktari tulipozungumza naye, presha ndio
linalozingua ,so far sasa hivi anaendelea vizuri kidogo,” alisema HK.
إرسال تعليق