Soma alichokisema H Baba kumhusu Marehemu Hanumba

kanumba-top

Siku ya kesho ni siku maalum kabisa ya kumkumbuka marehemu Steven Kanumba ( Kanumba Day ). Wasanii mbalimbali wa Bongo Movie na Bongo Flava wataungana na wananchi katika viwanja vya Dar Live kwa ajili ya kumkumbuka Kanumba.
Kanumba alikua msanii mwenye mafanikio sana na aliifanya tasnia ya filamu Tanzania kuweza kufanya vizuri sana katika Nchi za Afrika Mashariki. Alifanikiwa kupata tuzo mbalimbali ndani na nje ya nchi na ndio alikua msanii wa kwanza kabisa Tanzania kuweza kwenda Nigeria na kufanya movie na wasanii wakubwa nchini humo.
3dd0cedcb8ad11e3af60126a1d328eb2_8
Leo msanii H Baba kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka mambo mengi sana kumhusu Kanumba hasa jinsi alivyoweza kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu. H Baba aliandika “ Soma barua hii tafadhali? #kanumba nimfano bora wakuigwa katika Sanaa alijitolea kuipandika tasnia ya filamu tz uku akipigwa majungu makubwa nawapiga majungu wakuu … Alichokifanya yeye nikuziba masikio yake nakufanya jema ili kuifikisha tasnia yafilamu kupata thamani yajuu nawatanzania kupenda vya kwao wakasau filamu zanje .#kazikwa namaelfu ya watu msiba wake ulikuwa wakidunia kwasababu waliomfahamu #Stiven kanumba Niwengi kuliko aliowagahamu yeye kiukweli Sanaa inatupa heshima kubwa sana pasipo sisi wasanii kujielewa.. Wasanii tulijifunza mengi kutoka Kwa marehemu #kanumba alipigana nakuimba Wimbo ambao ulikuwa gumzo sana Kwa zile tungo alizoandika umo ndani je ? Viongozi wakiserikali mmejifunza nini kupitia Thamani ya Msanii apa Tanzania . Najua ata mie napigwa majungu makubwa ila Namwachia mungu Nawasii wasanii tupendane na muungano ndo silaa yetu wasanii mafungu ndo ujinga wetu wasanii . Kunawatu wanaishi kwakugombanisha wasanii ili wao wapitishe upumbavu wao kwenye tasnia ya Sanaa Tanzania . #BASATA nawapongeza Kwa juhudi zenu japokuwa wapo wasanii wanaotambua umuhimu wenu nawapo wasiojua umuhimu wenu ? #Bongo movie club nawapongeza sana ila msisahau #TAF ndo baba wa filamu Tanzania Nawaomba muonyeshe mapinduzi namuungano wenu kuipandisha tasnia ya filamu Tanzania ifike kule Kanumba alipotaka kuifikisha Acheni majungu pigeni Kazi namuungano ndo silaha yetu wasanii sina Mengi japo namengi Sikliza Wimbo wa #h.baba ft Pasha Utaelewa nini namaanisha Wimbo unaitwa (Thamani yetu) tuungane kwapamoja kuudhulia tamasha la Kanumba day? Ushirikiano nimuhimu sana Acheni Majungu kwani tunapotoshwa nawatu ili wafanye upumbavu waoooo Mazishi yakamarehemu Kanumba nihistoria tosha Kwa wasanii wamejifunza nini? Waigizaji na wanamuziki jifunzeni kwawaliotutangulia Mbele za haki akuna muziki wala filamu tukumbuke Kuswali mwenyezi atatusaidia?”

Post a Comment

أحدث أقدم