
****
Askari wa jadi maarufu kama sungusungu wa mtaa wa Mwatulole kata ya Kalangalala mjini Geita wanadaiwa kumdhalilisha na kumfanya ukatili mwanamke mmoja kwa kumkamata na kumcharaza viboko kwa tuhuma za kuvaa nguo fupi (kimini).
Inadaiwa
kuwa walichukua uamuzi huo baada ya kamanda wao kuwaamuru na kutangaza
sheria binafsi ya kuzuia watu kuvaa vimini kwenye mtaa huo.
Akizungumzia
kwa masitikiko mwanamke huyo, Jennifa Nobo (24) alidai kuwa
alishambuliwa na sungusungu hao Aprili 15, mwaka huu katika mtaa huo
wakati amekwenda sokoni.
Jeniffa
alisema kuwa alipokwenda sokoni hapo kununua mahitaji ya nyumbani
kwake, alikutana na sungusungu hao wakiwa wameongoza na kamanda wao
huyo, Daud Kulola.
Alidai
baada ya kukutana nao, walimkamata, kumpapasa maungoni wa kumhoji
sababu za kuvaa kimini ndani na juu khanga wakati kiongozi wao amepiga
marufuku kuvaa mavazi hayo katika mtaa huo.
Jeniffer
alidai bila kusikilizwa utetezi wake, sungusungu hao walianza
kumcharaza viboko hadharani na kumfuata kila alikokuwa akimbilia.
Alidai
wakati wakicharaza viboko walimbakiza na kimini hicho. Aliendendelea
kudai kuwa kamanda huyo alipochoka kumuadhibu, alimrejeshea khanga
yake.
''Nlilipita
kila kona akanifuata na kunicharaza kwa fimbo nililia sana na kutokwa
na haja ndogo kwa hofu na kipigo ..kilikuwa kitendo cha kinyama
ambacho sijawahi kutendewa katika maisha yanguna, sitakisahau,
''alidai..
Baadhi
ya wakazi wa mtaa huo walidai kuwa siku moja kabla ya tukio hilo la
ukatili, Kamanda huyo alisikiska akitumia kipaza sauti akitangaza kuwa
vijana na wasichana wote wake kwa waume wanaovaa vimini ni marufuku
kuonekana mtaani.
Walidai wengi wao walidhani huenda lilikuwa ni agizo la Serikali.
Baada
ya tukio hilo Jeniffa alikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi cha
Geita kufunguliwa jalada GE/RB/2033/ 2014 la shambulio la kudhuru mwili
kisha kupatia PF3 kwa ajili ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya
Wilaya ya Geita.
Alisema baadaye polisi walimkamata kamanda huyo wa sungusungu na kuachiwa kwa dhamana na kwamba uchunguzi dhidi yake unaendelea.
Kamanda huyo alikataa kuzungumzia madai hayo dhidi yake.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo, Kalori Malicery amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kukataa kuzungumzia kwa undani kwa madai
limeripotiwa polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alionyesha kusikitishwa na tukio hilo na kuahidi kuzungumzia leo ofisini kwake.
Konyo alisema kuwa iwapo ushahidi utathibitika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani.
إرسال تعليق