Baada
ya mvua kunyesha kwenye jiji la Dar es salaam na kuleta maafa, vifo,
hasara nyingine pamoja na foleni kubwa, Kamanda wa kikosi cha usalama
barabarani Mohammed Mpinga ameongea na millardayo.com kuhusu foleni na
barabara zilizokua zimefungwa.
Anasema >> ‘April 14 2014
jioni majira ya saa kumi na mbili na nusu pale Ruvu darajani kazi ya
kufanya marekebisho imekamilika ambapo magari mengi yameanza kupita
yakiwemo Malori na tayari tumekubaliana na RPC Pwani kwamba magari
yanaweza kuanza kupita kama kawaida’
‘Tumesharuhusu kuendelea na safari mabasi ambayo yanataka kwenda
Morogoro na safari nyingine zikiwemo za kutoka kituo kikuu cha Ubungo,
vilevile kulikua na magari mengine yamekwama pale Morogoro nayo tumesha
waelekeza wayaruhu kuendelea na safari ya Dar es salaam manake ni
shwari’
‘Kuanzia April 15 2014 kwa barabara hiyo hali ya usafiri itarudi kama kawaida, marekebisho yamekamilika vizuri kabisa’
‘Kuhusu daraja la Visiga pale wameshakamilisha mapema kabisa na pako
safi magari yanapita ila kwenye njia ya kusini mto Mzinga kwenye lile
daraja lililobomoka na kunyima magari kupita, April 13 2014 walianza
kuweka mawe na vifusi na jioni hii nimekwenda pale magari madogo tu ndio
yanaweza kupita’
Daraja jingine linalounganisha Kongowe kwenda Kigamboni kupita kwenye
mto Mkokoti, pale bado jitihada zinafanyika kuparekebisha kwa sababu
gari hazipiti hususani za mafuta ambazo huwa zinafanya safari za
Kigamboni lakini watu wa kawaida wanavuka kwa sababu sasa hivi hakuna
maji’
‘Juhudi
zinazofanyika ni kunyonya mafuta kwenye Lori lililoanguka pale ili
walinyanyue na tayari taratibu za kulinyanyua zimesha anza’
Kuhusu msongamano wa magari Dar es salaam April 14 2014, hii
ilisababishwa na kufungwa kwa barabara kati ya Fire na taa za Magomeni,
watumiaji wote wa barabara Dar es salaam wafahamu tu kuanzia sasa njia
hiyo imefunguliwa na inatumika kama kawaida, kesho (April 15 2014)
wapite njia zao za kawaida kasoro ile njia ya kupita Jangwani mpaka
roundabout ya Kigogo ndio bado haijafunguliwa ila Morogoro road
inatumika kama kawaida’
إرسال تعليق