Telephone : 255-22-2114512, 2116898
E-mail : ikulumawasiliano@yahoo.com
E-mail : press@ikulu.go.tz
Fax : 255-22-2113425
E-mail : ikulumawasiliano@yahoo.com
E-mail : press@ikulu.go.tz
Fax : 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za
rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa Paschal Mabiti,kuomboleza
vifo vya watu 11 ambao wamepoteza maisha yao katika ajali ya basi
iliyotokea mkoani humo leo, Jumatatu, Aprili 21, 2014.
Katika salamu hizo, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la
kusikitisha kuwa ajali zabarabarani zinaendelea kuchukua maisha ya watu
wasiokuwa na hatia.
“Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya ajali hiyo ambayo
nimejulishwa kuwa imetokea katika Kijiji cha Itwimila katika Wilaya ya
Busega katika Mkoa wako wa Simiyu wakati basi lililokuwa linasafiri
kutoka Tarime, Mkoa wa Mara kwenda Mwanza kupitia Simiyu lilipoacha njia
na kugonga nyumba kabla ya kupinduka.”
Amesema Rais Kikwete: “Nakutumia salamu zangu za
rambirambi na najiunga nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika
nchi yetu. Aidha, kupitia kwako, natuma salamu za dhati ya moyo wangu
kwa familia zote ambazo zimepoteza wapendwa wao katika ajali hiyo.
Naungana nao katika kuomboleza wapendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba
wao ni msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu,
Mwingi wa Rehema aziweke peponi roho za marehemu.”
Rais Kikwete vile vile ametoa pole kwa wote ambao wameumia katika
ajali hiyo, akiwaombea wapone haraka na kurejea kwenye shughuli zao za
kujiletea maendeleo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Aprili,2014

إرسال تعليق