![]() |
| Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema |
Na Dina Ismail, Dar es Salaam
KITENDO
cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukifuta kipengele kipya cha 26
cha Katiba mpya ya Simba SC na kurejesha kipengele cha zamani, ni
kinyume cha ushauri wa kitaalamu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, BIN
ZUBEIRY imebaini.
TFF
ilidai pendekezo la wanachama wa Simba kubadili kipengele na 26 kuhusu
sifa za mgombea kinapingana na kipengele na 29 (4) cha Katiba ya TFF,
ikaagiza kipengele cha zamani kibaki vilevile bila kubadilishwa.
Lakini
habari za kiuchunguzi, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata ni kwamba, TFF
ilimuandikia barua Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
kuomba ufafanuzi juu ya kipengele hicho.
Hatua
hiyo ya TFF ilifuatia barua waliyoandikiwa na wanachama wao, Chama cha
Soka Pwani (COREFA) ikipinga kipengele 29 (4) cha Katiba ya TFF.
Barua
ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenda TFF imeunga mkono ombi
la COREFA na kusistiza kuwa kipengele hicho ni kinyume cha utangulizi wa
Katiba yao wenyewe TFF, CAF, FIFA na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
kwamba kumbagua au kumtenga yeyote ni makosa, hivyo itabidi Msajili wa
Vyama vya Michezo ahakikishe Katiba zote za klabu na vyama hazipingani
na Katiba ya nchi.
Maana
yake- hata TFF pia watalazimika kufanyia marekebisho Katiba yao, juu ya
kipengele hicho kinachopingana na Katiba ya nchi kwa mujibu wa barua ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kwa
ushauri huo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali- ina maana baada ya TFF
kukiondoa kipengele kipya cha 26 cha Katiba ya Simba SC, inaweza kukwama
kupitishwa na Msajili wa Vyama na klabu za Michezo nchini.
Juhudi
za kumpata Rais wa TFF, Jamal Malinzi kuzungumzia suala hilo
hazikufanikiwa kwa kuwa bado yupo Afrika Kusini kwenye semina ya
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), pamoja na Katibu wake, Celestine
Mwesigwa na Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi.
TFF iliagiza mchakato wa uchaguzi wa Klabu ya Simba uendelee kama ulivyopangwa wakizingatia uamuzi huo, wakati huo huo Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji iliishauri TFF kuwasiliana na FIFA kupata mwongozo kuhusu katazo la watu wenye rekodi ya kifungo kugombea.
TFF iliagiza mchakato wa uchaguzi wa Klabu ya Simba uendelee kama ulivyopangwa wakizingatia uamuzi huo, wakati huo huo Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji iliishauri TFF kuwasiliana na FIFA kupata mwongozo kuhusu katazo la watu wenye rekodi ya kifungo kugombea.

Post a Comment