Timu ya mpira wa miguu ya Watoto wa Mtaani ya Tanzania iliyotwaa
kombe la dunia kwa watoto wa mtaani leo imetinga bungeni na kupongezwa
na bunge kwa kuipa heshima Tanzania.
Akizungumza leo bungeni wakati wa matangazo, Makamu Mwenyekiti wa
Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan amesema bunge linaipongeza
timu hiyo ya watoto wa mitaani kwa kuchukua ushindi huo pamoja na
kuitangaza Tanzania. Pia mmoja ya wajumbe wa bunge hilo ametoa hoja kwa
wabunge kuichangia timu hiyo ili kuisaidia zaidi.
Timu hiyo ilitwaa kombe la dunia kwa watoto wa mtaani baada ya
kuilaza timu ya Burundi mabao 3-1 kwenye fainali iliyopigwa jijini Rio
de Janeiro nchini Brazil.
إرسال تعليق