0
Wewe
kama mwanafunzi una vitu vingi vya kufanya, masomo, mitihani, kufurahi
pamoja na wenzako, ni ngumu kuanza kitu kingine ukiongezea kwenye
masomo. Si kana kwamba kuanza biashara ukiwa chuoni ni rahisi ila
inakusaidia kuweka msingi wa kibiashara kama unataka kuendeleza taaluma
yako ya biashara. Ukiwa chuoni unatengeneza mtandao wa watu ambao
utawatumia baadaye, utashirikiana nao na vile vile kujiimarisha kifedha.
1. Wanafunzi hutoa huduma bora na kwa bei poa kabisa
Chuoni
ni sehemu ambayo kila mtu anajifunza, uko darasani na watu walewale
kila wakati. Hivyo unapokaribia kumaliza una watu ambao unawaamini na
unajua uwezo wao wa kufanya kitu fulani hivyo unawatumia kirahisi au kwa
bei nafuu kuliko ungetafuta mtu ambaye hayupo chuoni mwenye uwezo kama
huo huo. Wengine wana uwezo wa kukusaidia bure kimawazo hata kufanya
baaadhi ya mambo wakati wewe ndo unaijenga hiyo biashara. Hii
inakusaidia kuendelea kujifunza pamoja nao na kujenga team hivyo
kupunguza gharama za mishahara.
2. Fursa ya kifedha, zaidi ya vile unavyojua!
Tunaishi
kwenye ulimwengu wa kunywa pombe na anasa mbalimbali, mitindo tofauti
tofauti ya mavazi n.k . Hivyo ukitengeneza wazo lako na ukaamua
kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima unajikuta una mtaji wa kuanza
kitu kidogo hapo hapo ulipo. Kama unasomeshwa au kupewa mkopo na
serikali unakuwa na uwezo wa kubana matumizi na kufanya kitu cha
tofauti, jaribu kuangalia wanafunzi wenzako wanavutiwa na nini kila
siku, au ni kitu gani ambacho wanakilipia kila siku na kama unaweza
kupata kwa bei rahisi na wewe ukatengeneza faida hapo hapo. Uko eneo la
soko ambalo haliingiliwi sana kuliko mtaani ambako ushindani ni mkubwa.
3. Unapata ushauri wa bure kutoka kwa wataalamu
Kila
mfanyabiashara ambaye alianza akiwa mdogo atakwambia umuhimu wa kuwa na
mtu wa kukushauri. Hivyo ukiingia kwenye ulimwengu wa kawaida tofauti
na chuo unataingia kwenye biashara yenye matatizo mengi na ushindani
mkubwa huku ukikosha washauri wazuri. Bali unapokuwa chuoni washauri
wengi hupenda kutoa hizo huduma bure kwa wanafunzi ili kujitangaza na
kusaidia wanafunzi kwa namna moja ama nyingine. Usipuuzie hao watu maana
utakapotoka chuoni inakuwa ni vigumu kuwapata.
4. Shida sio kushindwa
Sio
mara zote biashara zinafanikiwa, ila unapoanza mapema na huku
unaendelea na masomo madhara yake sio makubwa sana kuliko ukiwa nyumbani
unafanya biashara hiyo hiyo halafu ikakushinda. Unapoendelea kujifunza
unatengeneza taaluma yako ya baadaye kibiashara. Watu wengi watategemea
ushindwe, ila kushindwa huko kunakuongezea uzoefu wa kufanya na kuepuka
makosa baadaye. Unahitaji ubunifu na kutokukata tamaa pale mambo
yanapokuwa hayaendi vizuri.
5. Tengeneza cheo cha kazi unachotaka wewe
Unapoanza
kufanya biashara yako , wewe ndio msemaji wa mwisho. Ungependa watu
wakutambue kama nani kwenye biashara yako? Lakini inakupa kujitengenezea
kazi unayoitaka hasa katika maisha yako, ambayo ungeamua kujiajiri
ingekutumia muda mrefu kuja kuifikia.
6. Tafuta kitu unachokitaka
Watu
wengi hukimbilia biashara baada ya kumaliza chuo bila kuwa na elimu
yeyote au ufahamu wa mambo ya biashara. Kitu ambacho huwafanya kupoteza
fedha nyingi na muda, hivyo unapokuwa chuoni jifunze kupitia mafunzo
madogo madogo yanayohusu biashara na ufanyie utafiki na mazoezi namna ya
kufanya hizo biashara. Ili utakapotoka chuoni ujue ni jambo gani hasa
unataka kuliendeleza kibiashra baada ya kujifunza na kujaribu aina
mbalimbali za biashara ukiwa chuoni. Hivyo utajikuta unatengeneza
taaluma ambayo ndio yatakuwa maisha yako hapo mbeleni.
إرسال تعليق