
Berlin,Ujerumani,
Umoja
wa Watanzania Ujerumani (UTU) unatarajia kufanya mkutano wake mkuu wa
uchaguzi siku ya kilele cha sherehe za muunganno wa Tanzania mjini
Berlin, Ujerumani. siku ya tarehe 26.April.2014 kuanzia saa 7 mchana
katika ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117 Berlin,
Ujerumani.
Agenda za Mkutano
1 Uchaguzi wa Viongozi
2 Kuipitisha Katiba Mpya
Kwenye
Attachments nimeweka Katiba ya zamani, na katiba mpya Satzung na
satzungentwürf tafadhali pitia katiba hizi ili tuone mabadiliko hayo
ili kuepuka kutumia muda mwingi katika kujadili.
Watanzania
wote wanaoishi Ujerumani wanaombwa kuhudhuria kwa wingi katika mkutano
huu muhimu wa chombo chao UTU ambao kinawaunganisha watanzania wote
waishio ujerumani bila kujali itikadi zao za kidini, jinsia, wala
kabila.
Umoja wa watanzania ujerumani unafuraha kubwa ya kuwafungilia milango wale wote ambao wanataka kujiunga na umoja huo.
KUFIKA KWENU KATIKA MKUTANO HUU NDIO MAFANIKIO YA WATANZANIA WOTE
UMOJA NI NGUVU , UTENGANO NI UDHAIFU
UMOJA WA KITAIFA NDIO MSINGI IMARA KWA WATANZANIA
MUNGU IBARIKI TANZANI
Kwa maelezo zaidi wasiliana simu : +491737363422
Email. kamati.utu@googlemail.com
إرسال تعليق