Baraza la Usalama la Umoja wa
mataifa limepiga kura kwa kauli moja kutuma kikosi kipya cha wanajeshi
wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati-kikosi hicho
kitawajumuisha wanajeshi karibu alfu kumi na mbili.
Kwa sasa kuna wanajeshi alfu sita wa kikosi cha
umoja wa Afrika pamoja na alfu mbili kutoka Ufarnsa, lakini vikosi hivyo
vimekabiliwa na wakati mgumu kurejesha utulivu.Maelfu wamefariki duniani na takriban watu milioni moja wamelazimika kutoroka makwao kufuatia vurugu zilizodumu kipindi cha mwaka mmoja sasa.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, anasema kuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati inakabiliwa na mzozo unaoibua wasiwasi-- ambapo wanamgambo wa mirengo pinzani ya kidini wanaendelea kupigana huku msimu wa mvua unaotarajiwa kuanza ukitishia zoezi la kusambaza misaada kwa waathiriwa.
Zaidi ya raia thelathini waliuwawa katika mapigano ya hivi punde katika mji wa Dekoa katikati mwa taifa hilo.
إرسال تعليق