![]() |
| Mgambo JKT |
![]() |
| Ashanti United |
BAADA ya Azam kupata ushindi wa mabao
2-1 na kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara bila kupoteza mchezo
wowote, huku Yanga ikishinda mjini Arusha kwa idadi kama hiyo, vita kwa
sasa ipo kwa timu zilizopo mkiani, baada ya Mgambo JKT leo kulazimishwa
suluhu kwenye uwanja wa Mkwakwani na Kagera Sugar na kuwafanya wasipumue
vyema.
Sare hiyo imeifanya timu hiyo kufikisha
pointi 26 moja zaidi ya timu za Ashanti United iliyoinyoa Simba jijini
Dar es Salaam na Prisons iliyoishusha daraja Rhino Rangers mjini Mbeya
jana kwa kuilaza mabao 4-3 ambazo kila moja ina pointi 25 baada ya mechi
25 kwa kila timu.
Timu mojawapo kati ya hizo zitaungana na
Rhino Rangers na Oljoro JKT iliteremsha leo kurudi Ligi Daraja la
Kwanza na Mabingwa watetezi Yanga kwa kufungwa 2-1 kuzipisha timu za
Polisi Moro, Ndanda Fc ya Mtwara na Stand United ya Shinyanga
zilizopanda Ligi Kuu kwa msimu ujao.
Mechi za Jumamosi hasa inayozikutanisha
AShanti United na Prisons mjini Morogoro ndiyo inayosubiriwa kwa hamu
kuona inakuwaje kwa timu hizo zilizorejea ligi kuu kwa misimu miwili
tofauti.
Pia kama Simba itaendelea kutoa takrima
kwa wapinzani wake kuna uwezekano ikajikuta ikitolewa kwenye nafasi ya
nne iliyoikalia kwa muda mrefu kutokana na Kagera Sugar na Ruvu Shooting
kuonekana kuinyemelea nafasi hiyo nyuma yao.
Hapa chini ni msimamo kamili baada ya mechi za leo za ligi hiyo;
P W D L F A D Pts
1.Azam 25 17 8 0 50 15 +35 59
2.Yanga 25 16 7 2 60 18 +42 55
3.Mbeya City 25 12 10 3 32 20 +12 46
4.Simba 25 9 10 6 40 26 +16 37
5.Kagera Sugar 25 8 11 6 22 20 +2 35
6.Ruvu Shooting25 9 8 8 26 32 -6 35
7.Ruvu Stars 25 10 1 14 23 39 -16 31
8.Mtibwa Sugar25 7 9 9 29 30 -1 30
9.Coastal Union25 6 11 8 16 19 -3 29
10.JKT Mgambo25 6 8 11 18 34 -16 26
11.Prisons 25 5 10 10 25 33 -8 25
12.Ashanti Utd 25 6 7 12 20 38 -18 25
13.JKT Oljoro 25 3 9 13 18 36 -18 18
14.Rhino Rangers25 3 7 15 18 37 -19 16


إرسال تعليق