
Kocha Msaidizi wa Taifa Stars Salum Mayanga ametangaza wachezaji
wengine 23 watakaoingia kambini kesho Aprili 20 kuungana na 16
waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi ambayo
itachezwa Aprili 26 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam),Deogratias Munishi
(Yanga) na Mwadili Ali (Azam) upande wa mabeki ni Abdi Banda (Coastal
Union),Aidan Michael (Ruvu Shooting),Aggrey Morris (Azam),Erasto Nyoni
(Azam),Hassan Mwasapili (Mbeya City),Kelvin Yondani na Said Moradi
(Azam).
Upande wa Viungo ni Amri Kiemba (Simba),Frank Domayo (Yanga),Himid
Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba)na Washambuliaji ni Athanas Mdamu
(Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis
Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga),
Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva
(Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa
Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda
(Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari
Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz
Abdallah Sozigwa (Ilala).
Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini
Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan
Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito
(Manyara).
Washambuliaji niMohammed Seif Saidi (Kusini Pemba),Ayoub Kasim Lipati
(Ilala),Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi),Paul Michael Bundara
(Ilala). Wachezaji wa U 20 niMbwana Mshindo Musa (Tanga) naBayaga
Athanas Fabian (Mbeya).
Taifa Stars inategemewa kuingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.
إرسال تعليق